Son Peygamber Çocuk 🌳 Mwanzo
Instagram Twitter Facebook
  • 571
  • 571
  • 574
  • 575
  • 577
  • 589
  • 594
  • 594
  • 605
  • 610
  • 610
  • 613
  • 614
  • 615
  • 616
  • 620
  • 620
  • 621
  • 621
  • 622
  • 622
  • 622
  • 622
  • 622
  • 622
  • 622
  • 622
  • 623
  • 623
  • 623
  • 624
  • 624
  • 624
  • 624
  • 624
  • 624
  • 624
  • 624
  • 624
  • 625
  • 625
  • 625
  • 626
  • 627
  • 628
  • 628
  • 628
  • 628
  • 628
  • 628
  • 629
  • 630
  • 630
  • 630
  • 630
  • 630
  • 631
  • 632
  • 632
  • 632
  • 571

    Bwana Mtume (S.A.W.) – Allah amshushie rehma na amani azaliwa na kupewa jina Muhammad.

  • 571

    Bibi Halima alifurahishwa sana kupewa Bwana Mtume (S.A.W.) kuishi naye akimnyonyesha.

  • 574

    Bwana Mtume (S.A.W.) alikuzwa na maziwa ya Bibi Halima na akarudishwa kwa mama yake mzazi Bibi Amina ilhali akiwa amekuwa kabisa.

  • 575

    Mamaye Bwana Mtume (S.A.W.) alipofikwa na mauti, Bwana Mtume (S.A.W.) alihamia kwa babu yake aliyempokea kwa mikono miwili.

  • 577

    Baada ya babu yake naye kufariki, Bwana Mtume (S.A.W.) alianza kuishi na mjomba wake. Alifanya safari nyingi akiwa na mjomba wake akiwa mwenye kujifunza kazi ya biashara toka kwake.

  • 589

    Akiwa mjini Makkah Bwana Mtume (S.A.W.) alikuwa pamoja na watu wema walioishi pale katike enzi hizo. Alishiriki pia katika Ushirikiano wa Hilf al Fudu’l.

  • 594

    Bwana Mtume (S.A.W.) alikuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa. Alikuwa akipeleka misafara mikubwa yenye shehena za biashara kwenda katika mji wa Busra. Alionyesha umahiri mkubwa katika kufanikisha shughuli hii.

  • 594

    Bwana Mtume (S.A.W.) alimwoa Bibi Khadija (R.A.). Bibi Khadija (R.A.) alikuwa akimpenda sana Bwana Mtume (S.A.W.) na pia alikwa wa kwanza kumwaminia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

  • 605

    Al Kaaba ilikuwa sehemu inayoheshimiwa sana hata kabla ya Uislamu. Hajar al Aswad, yaani Jiwe Jeusi lilikubalika kama alama iliyo tukufu kabisa. Katika kukarafati jumba hili tukufu aghalabu makabila yaliyekuwepo Makka enzi hizo yalighalifiana juu ya nani hasa aliweke sawa jiwe hili. Wakati ambapo ilikuwa imebaki chembe tu makabila yapambane kutokana na ubishani huu, Bwana Mtume (S.A.W.) aliingilia kati na kuwanasihi mahasimu namna ya kulibeba jiwe lile kwa pamoja na kuepuka umwagaji damu ambao ungetokana na malumbano haya.

  • 610

    Akiwa katika Jabali la Hira, Bwana Mtume (S.A.W.) alikutana na malaika aliyempa zawadi ya kitabu. Kitabu hiki chenye uongozi wa binadamu wote ndiyo Kur’an Takatifu.

  • 610

    Aya za mwanzo kabisa katika Kur’an Takatifu zinaarifu kwa Bwana Mtume (S.A.W.) na binadamu wote, zikisema: “Soma” “Soma! Kwa jina la Mola wako Aliyeumba, Amemuumba binadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola Wako Mlezi ni Karimu kupita wote. Ambaye Amefundisha kwa Kalamu. Kamfundisha Mtu yale aliyokuwa hayajui”

  • 613

    Allah (S.W.) Alimfundisha Bwana Mtume (S.A.W.) na kumwamuru awaarifu na walio karibu naye. Alimweleza ayaseme kwa uwazi yale yaliyo kweli. Haipasiki kuficha yaliyo hakika.

  • 614

    Siku ngumu zilikuwa zikiwasubiri waliomwamini Bwana Mtume. Kwani wasioamini hawakuwapa nafasi, waliwabana wasipate fursa ya kuamini. Hawa wasioamini walifanza uadui aina mbali mbali dhidi ya waumini.

  • 615

    Waumini waliobanwa na kusakamwa sana mjini Makkah walifanya hijra ya mwanzo kabisa. Waliondoka mjini Makka na kuelekea Uhabeshi.

  • 616

    Katika kila mji palikuwa mashujaa waumini. Miongoni mwa mashujaa hodari wa Makka walikuwepo Bwana Hamza (R.A.) na Bwana Omar (R.A.). Hawa walikuwa na nguvu nyingi. Waliposilimu kuwa waislamu, nguvu ya waumini iliongezeka maradufu. Waumini wakawa mashujaa wasio uwoga kabisa.

  • 620

    Hakika Abu Talib alikuwa mjomba aliyekuwa mithili ya baba kamili kwa Bwana Mtume. Alipofariki Abu Talib, Bwana Mtume (S.A.W.) akawa amepoteza nguzo iliyokuwa na nguvu aliyeitegemea sana. Mara baada ya hapo kipenzi cha Bwana Mtume, mkewe Bibi Khadija (R.A.) naye akashikwa na umauti. Mwaka huo ulijawa na huzuni kubwa kwa Bwana Mtume (S.A.W.) tokea mwanzo. Waislamu wanaukumbuka mwaka huu wakiuita “Mwaka wa Huzuni”.

  • 620

    Bwana Mtume (S.A.W.) aliwaarifu mahujaji tokea miji ya jirani kuhusu Uislamu. Kikundi toka Madina kilimwamini kabisa Bwana Mtume (S.A.W.) mara walipokutana naye (Agano la Kwanza la Aqaba).

  • 621

    Siku hizi zilikuwa ngumu na zenye hati hati. Milango yote ya fursa katika mji wa Makkah ilionekana ikifungwa machoni mwa waumini. Ni katika kipindi hiki ambapo tukio la ajabu kabisa lilipotokea. Katika mazingira ya kimiujiza Bwana Mtuma alifanya “Safari ya Usiku”. İlikuwa wakati wa usiku ambapo Bwana Mtume (S.A.W.) aliposafiri toka Masjid Haram na kufika Masjid Aksa kwa kipindi cha kufumba na kufumbua. Akiwa Masjid Aksa alikutana na Mitume iliyopita kabla yake. Baadaye akakwezwa kufikia kiwango cha mwisho kabisa ambacho binadamu yoyote mwingine asingeweza kamwe kufikia. Hapo Bwana Mtume (S.A.W.) alwasiliana na Allah (S.W.) kwa namna mahsusi kabisa. Allah (S.W.) Akawazawadia waislamu swala kama njia ambayo kwayo wataweza kukwezwa kumkurubia Mwenyezi Mungu Allah (S.W.) Ukweli swalah ni mithili ya ngazi za kupanda kuelekea mbinguzenye daraja kubwa.

  • 621

    Mus’ab (R.A.) ndiye mwalimu wa kwanza wa Uislamu. Alisafiri hadi Madina ili kuwafundisha waumini namna ya kuishi kiislamu.

  • 622

    Wakazi wa Madina walichagua Uislamu kama namna yao ya maisha. Karibia wawakilishi wote wa mji walitakabalia Uislamu kwa pamoja (Agano la Pili la Aqaba).

  • 622

    Mji wa Madina ikawa kama mama anayetabasamu. Ukawapokea waliohamia kwa mikono miwili. Ili kuishi kiislamu kwa ukamilifu na furaha zaidi waislamu walianza kuhamia Madina kwa wingi.

  • 622

    Maadui wa Uislamu walidhania kuwa wakimuua Bwana Mtume (S.A.W.) aliyekuwa mpweke pale Makkah basi watakuwa wamefanikiwa kuumaliza Uislamu. Kwa sababu hii katika kikao chao kiovu waliamua namna ya kumuua Bwana Mtume.

  • 622

    Akiwa na Bwana Abubakar (R.A.) aliyekuwa swahaba yake wa karibu kabisa, Bwana Mtume (S.A.W.) alisafiri kuelekea Madina. Wakiwa njiani walijihifadhi kwa muda katika pango liitwalo Seyr.

  • 622

    Bwana Mtume (S.A.W.) alipofika mjini Kuba akiwa njiani kuelekea Madina alijenga msikiti mdogo.

  • 622

    Alipowasili Madina Bwana Mtume (S.A.W.) kwa mara ya kwanza aliswalisha swala ya Ijumaa. Katika khutba aliyotoa aliongelea umoja na ushirikiano. Ilikuwa kama anayesema “Kwa pamoja tutakuwa binadamu wazuri kabisa”.

  • 622

    Mjini Madina palijengwa msikiti kwa jina la Bwana Mtume (S.A.W.).

  • 622

    Ili kuwaita waumini kwa swalah ilionekana vema ipigwe adhana. Kwa waislamu, ipigwapo adhana basi wao huharakia swalah kana kwamba wanamkimbilia Allah (S.W.). Ama kwa hakika swalah ni kipindi mahsusi cha mja kukutana na muumba wake, Mwenyezi Mungu Allah (S.W.).

  • 623

    Wakazi wa Madina waliwakaribisha na kuwakarimu wageni toka Makka kwa mikono miwili na moyo mmoja.

  • 623

    Upande mmoja wa msikiti wa Bwana Mtume (S.A.W.) uligeuzwa shule. Katika kitengo hiki waliotaka kujiendeleza zaidi juu elimu ya dini walijiunga kuwa wanafunzi wa Bwana Mtume. Naye Bwana Mtume (S.A.W.) alikuwa mwanafunzi wa Allah (S.W.).

  • 623

    Kwa mara ya kwanza waislamu walilazimika kupigana vita. Katika vita vya Bedir maelfu ya malaika walishiriki kuwasaidia waumini kushinda.

  • 624

    Al Kaaba yawa kibla kwa waislamu.

  • 624

    Swaumu yafaradhishwa katika mwezi huu. Kuanzia hapa waislamu watafunga katika mwezi mzima wa Ramadhani na katika kukabiliana na ugumu wa swaumu watajifunza namna ya kufanya subira.

  • 624

    Moja kati ya mawaridi ya Bwana Mtume (S.A.W.) latoweka. Kipenzi bintiye Rukiyyah (R.A.) afariki.

  • 624

    İli kusaidia wasiojiweza, hususan wakati wa sikukuu ya Idi imeamuriwa utoaji wa Sadakat Fitri.

  • 624

    Baada ya kukamilisha mwezi wa ibada waumini wanazawadiwa sikukuu ya Idi. Katika sikukuu hii waumini wanakutana na pamoja wanswali swalah ya Idi.

  • 624

    Bwana Mtume (S.A.W.) amwoa Bibi Aisha (R.A.).

  • 624

    Bwana Mtume (S.A.W.) amwoza bintiye Fatuma (R.A.) kwa Bwana Ali (R.A.) aliyemlea tangia akiwa mtoto mdogo.

  • 624

    Kwa mara ya kwanza sikukuu ya Idi el Adha inasherehekewa. Ni katika kipindi hiki ambapo amri ya zaka inatolewa, yaani matajiri wanatakiwa kuwasaidia mafukara.

  • 624

    Bwana Athuman amwoa Bintiye Bwana Mtume (S.A.W.) aitwae Bibi Ummu Kulthum (R.A.).

  • 625

    Mjukuu wa kwanza kwa Bwana Mtume, Bwana Hasan (R.A.) azaliwa. Sasa Bwana Mtume (S.A.W.) anakuwa babu.

  • 625

    Vita ya Uhud vinatokea. Inabaki kidogo tu waislam kushindwa vita kutokana na kadhaa miongoni mwao kutokufuata ahadi walizotoa kwa Bwana Mtume.

  • 625

    Ulevi unapigwa marufuku kutokana na hasara unazoleta.

  • 626

    Bwana Mtume (S.A.W.) apata mjukuu wa pili kutokana na kuzaliwa kwa Bwana Husein (R.A.).

  • 627

    Mahandaki yachimbwa. Vita vinatokea na mahasimu wa uislamu wanashindwa kuvuka mahandaki haya na kwa hivyo wanashindwa kuwadhuru waislamu.

  • 628

    Ukame unatokea katika maeneo ya Madina. Bwana Mtume (S.A.W.) na maswahaba wake wanafanya du’a kuomba mvua.

  • 628

    Ziara zinafanywa Al Kaaba nje ya kipindi cha kuhiji. Ziara hizi zaitwa Umra na zinawasaidia waislamu kupunguza hamu yako kubwa kuzuru Al Kaaba.

  • 628

    Bwana Mtume (S.A.W.) anazuru maziarani kwa mama yake katika mahali panapoitwa Ebva.

  • 628

    Makubaliano makubwa ya mwanzo yafanyika pale Hudaybiya.

  • 628

    Sura ya Fat-h’i yashushwa. Sura hii inayoarifia msaada na ushindi inakuwa zawadi kubwa kwa waislamu.

  • 628

    Bwana Mtume (S.A.W.) awataka wote wamhimidie Allah (S.W.). Aomba du’a ili kila mmoja awe katika siratul mustakiin. Aandika barua zinazouarifia uislamu na kuwatuma wajumbe kuzipeleka mataifa yaliyo jirani. Wajumbe hawa wanakuwa mithili ya njiwa wanaowasilisha habari njema.

  • 629

    Waridi jingine la Bwana Mtume (S.A.W.) latoweka. Bintiye mpenzi, Bibi Zainabu (R.A.) aaga dunia.

  • 630

    Bwana Mtume (S.A.W.) arejea Makkah alipolazimika kundoka huko nyuma. Makka inatekwa na kuwa chini ya Dola la Kiislamu.

  • 630

    Bwana Mtume (S.A.W.) anakutana tena na Sheyma, nduguye wa kunyonya waliyecheza na kukua pamoja katika michanga ya jangwani wakiwa kingali watoto wadogo.

  • 630

    Tabuk, ambapo waumini walijaribiwa na adha kubwa na ushindi ukapatikana kwa wale waliofanya subira.

  • 630

    Ka’b bin Zuheir (R.A.) aliyekuwa mshairi mahiri kabisa katika enzi za Bwana Mtume (S.A.W.) asilimu. Bwana Mtume (S.A.W.) anamzawadia vazi alilokuwa akivaa mwenyewe mgongoni. Hii inaonyesha kiasi Bwana Mtume (S.A.W.) alitoa umuhimu kwa ushairi na sanaa kwa ujumla.

  • 630

    Lat, sanamu lililokuwa kubwa zaidi laangushwa na kuangamia toka nyoyoni. Hakika halikuwa na uhai wowote hata kabla.

  • 631

    Katika mwezi mtukufu wa Ramadhani Bwana Mtume (S.A.W.) aisoma Kur’an Takatifu mwanzo mpaka mwisho kwa mara mbili. Wakati huo huo Malaika Jibrili asoma naye kila aya pamoja na kwa usahihi kamili. Nasi tunasoma hatimu ya Kur’an Takatifu yote kipindi cha mwezi wa Ramadhani kama ukumbusho wa tukio hili.

  • 632

    Kwa sasa hakika Bwana Mtume (S.A.W.) ameshakuwa mtu mzima sana na uzee umemfikia. Awahutubia maswahaba wake kwa mara mwisho wakati wa msimu wa kuhiji. Hotuba hii hujulikana kwa jina “Hotuba ya Kuaga”.

  • 632

    Bwana Mtume (S.A.W.) atekeleza ibada yake ya kuhiji kwa mara ya mwisho. Azunguka jumba hili la Allah (S.W.) mara saba kwa hushui kubwa. Kuzunguka huku kunaitwa tawaf.

  • 632

    Bwana Mtume (S.A.W.) apatwa ugonjwa na kama ilivyo kwa kila binadamu akamilisha kipindi cha uhai wake. Azikwa katika makaburi ya Jannat ul Baki.

Copyright © 2026, Meridyen Derneği & Son Peygamber Çocuk. Tüm hakları saklıdır.